Mshambuliaji mkongwe Danny Mrwanda ameifungia Yanga bao pekee dhidi ya Polisi Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mrwanda alifunga bao hilo katika dakika ya 42 baada ya kumalizia mpira uliopigwa na Simon Msuva.
Mpira ulianzia kwa beki Juma Abdul aliyepiga krosi ambayo iliunganishwa kwa tik tak na Msuva, kipa wa Polisi Deo Kavishe akapangua lakini mpira ukamkuta Mrwanda aliyefunga kwa shuti la karibu.
Hata hivyo Yanga ilicheza soka bovu huku wakizidiwa uwezo wa umiliki wa mpira na Polisi Morogoro.
Yanga pia bado iliendelea kuonyesha ubutu wake katika safu ya ushambuliaji baada ya kupoteza nafasi chache za wazi za kufunga magoli.
Polisi Moro ilifanikiwa kutibua mipango ya Yanga na kufanya watoto hao wa Jangwani washindwe kabisa kucheza mpira wa kuonana.
Comments
Post a Comment