WILFRIED BONY SASA NI MALI YA MANCHESTER CITY …aanguka mkataba wa miaka minne



WILFRIED BONY SASA NI MALI YA MANCHESTER CITY …aanguka mkataba wa miaka minne

Uhamisho wa bei mbaya wa Wilfried Bony kwenda Manchester City kutoka Swansea umekamilika baada ya nyota huyo kusaini mkataba wa miaka minne na atavaa jezi namba 14 iliyokuwa inavaliwa na Javi Garcia.

Wilfried Bony ambaye  kwa sasa yuko na timu ya taifa ya Ivory Coast akijiandaa na michuano ya Africa Cup of Nations, anajiunga na kikosi cha Manuel Pellegrini kwa ada ya pauni milioni 25 huku pauni milioni 3 zikiongezwa kadri atakavyoieletea mafanikio City.

"Ni jambo lenye hisia kubwa sana kwangu, ni heshima kuwa pale, ni changamoto kubwa", alisema Bony mwenye umri wa miaka 26.

"Kwa mchezaji ni jambo zuri kuwa sehemu ya moja ya timu kubwa duniani na ni nafasi nzuri kwangu kuwa katika hali hiyo – Ninajisikia fahari sana."

Bony atalipwa kitita cha pauni 100,000 kwa wiki ambayo inakaribia kuwa mara mbili ya mshahara aliokuwa akilipwa Swansea.

Wilfried Bony (posing with Ivory coast president Sidy              Diallo) has completed his move to Manchester City



Comments