WAKATI WADAU WAKICHANGA NAULI ILI AREJEE DAR, KUMBE BANZA STONE ALISHAKULA NAULI YA MDAU MWINGINE …apiga chenga ya mwili Airport


WAKATI WADAU WAKICHANGA NAULI ILI AREJEE DAR, KUMBE BANZA STONE ALISHAKULA NAULI YA MDAU MWINGINE …apiga chenga ya mwili Airport
WAKATI WADAU WAKICHANGA NAULI ILI AREJEE DAR, KUMBE BANZA            STONE ALISHAKULA NAULI YA MDAU MWINGINE …apiga chenga ya mwili            Airport

Banza Stone huwa haishi vituko, kumbe angeweza kurejea Dar es Salaam kabla hata hajazidiwa huko Tunduma iwapo angeitendea haki nauli aliyotumiwa hapo awali.

Mwanamuziki huyo kipenzi cha wengi alikwama Tunduma baada ya kundi lao la Rungwe Music Band kufanya vibaya kwenye ziara yao ya mkoani Mbeya wakati wa msimu wa sikukuu ya Mwaka Mpya.

Banza alimpigia simu mdau mkubwa wa muziki wa dansi Yusuphed Mhandeni (Papaa Yusuphed) wa Dar es Salaam na kumuomba nauli ya kutoka Tunduma hadi Dar es Salaam.

Banza akatoa mjumuisho wa nauli kuwa ni shilingi 10,000 Tunduma hadi Mbeya na shilingi elfu 40 Mbeya hadi Dar es Salaam. Yusuphed akamtumia 70,000 siku ya tarehe 21 mwezi huu.

Wakati Banza akifanya mawasiliano na Yusuphed alikuwa sambamba na wanamuziki wenzake Athanas na Jua Kali.

Yusuphed ameiambia Saluti5 kuwa siku mbili baada ya kumtumia Banza pesa hizo, akajaribu kumtafuta Banza lakini hakumpata na alipoongea na kina Jua Kali ili kujua kama mwimbaji huyo kisharejea Dar, Jua Kali akamwambia: "Wee wacha tu, huyu jamaa haeleweki, hajaondoka."

Yusuphed amesema baadae alishangaa kusikia Banza yuko hoi na anachangiwa michango ya kurejea Dar. "Najiuliza ile elfu 70 aliifanyia nini?" anahoji Yusuphed.

"Wanamuziki wawe wakweli, waachane na tabia kunadi shida moja kwa watu tofauti tofauti hususan pale wanapokuwa wameshapata utatuzi kwa mtu wa kwanza.

"Mara kadhaa inatokea hivyo, msanii anakulilia shida ya jambo fulani, unamsaidia lakini baadae unagundua kuwa shida ile ilitatuliwa pia na watu wengine zaidi ya watatu …kama shida yake ilikuwa ni laki moja basi anajikusanyia laki nne za ujanja ujanja," aliongeza Yusuphed.

Katika hatua nyingine, Banza aliingia Dar es Salaam saa 4 asubuhi kwa ndege ya Fast Jest badala ya saa 8 mchna kama alivyosema, hii ikawa ni chenga ya mwili Dar es Salaam Airport.

Mmoja wa watu wa karibu wa Banza Stone ameiambia Saluti5 kuwa Banza alizuga kuhusu muda wake wa kuwasili Dar ili kukwepa kamera za waandishi na wadau.

"Banza aliwaficha hata wadau wa Dar es Salaam waliomsadia michango, hakuna aliyejua hadi alipofika nyumbani kwao Sinza," alisema rafiki huyo wa Banza.



Comments