Magoli kutoka kwa wachezaji Riyad Mahrez wa Leicester na Nabil Bentaleb wa Tottenham yaliipatia Algeria ushindi wa 2-0 dhidi ya Senegal na kutinga robo fainali ya Afcon 2015.
Senegal inaungana na Afrika Kusini katika kufungasha virago kwenye kundi C huku Algeria ikipenya sambamba na vinara wa kundi hilo Ghana iliyoifunga Afrika Kusini 2-1.
Algeria walikuwa na kiwango bora zaidi na haikushangaza pale wachezaji hao wawili wa Ligi Kuu ya England walipotupia mabao wavuni na kukata tiketi ya robo fainali.
Comments
Post a Comment