WAKALA WA FALCAO AMPONDA VAN GAAL, ASEMA BORA INGEKUWA MAN UNITED YA SIR ALEX FERGUSON


WAKALA WA FALCAO AMPONDA VAN GAAL, ASEMA BORA INGEKUWA MAN UNITED YA SIR ALEX FERGUSON

Radamel Falcao endured another miserable night in                front of goal in United's 0-0 FA Cup draw with Cambridge

Wakala wa Radamel Falcao, Jorge Mendes amemtupia dongo kocha wa Manchester United, Louis van Gaal kwa kudai kuwa anatamani mchezaji wake angecheza chini ya kocha enzi za Sir Alex Ferguson.

Nyota huyo wa Colombia amekuwa na wakati mgumu Old Trafford kufuatia uhamisho wake wa mkopo wa bei mbaya kutoka Monaco.

Falcao amefanikiwa kufunga mabao matatu tu katika mechi 13 za Premier League alizocheza na akashindwa kung'ara kwenye mechi ya FA Cup iliyoishia kwa sare ya kutofungana dhidi ya timu ndogo ya Cambridge United Ijumaa jioni.

Manchester United manager Louis van Gaal has only              played Falcao for a full 90minutes twice

Van Gaal amemtumia Falcao kwa dakika 90 katika mechi mbili tu, jambo linalomfanya Mendes ambaye ni wakala bingwa kusema kuwa ingekuwa bora kuwa chini ya Sir Alex Ferguson kuliko Van Gaal.

Mendes anadai kama Falcao mwenye umri wa miaka 28 angecheza Manchester United chini ya Ferguson basi magoli yangemiminika Old Trafford.



Comments