Kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdes anajiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza Manchester United Ijumaa hii dhidi ya Cambridge katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA.
Beki wa United Chris Smalling amesema makali ya kipa huyo yako pale pale na watu watarajie mengi mazuri kutoka kwake.
Louis van Gaal amedhamiria kumpa nafasi kipa huyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipokamilisha usajili wake wa miezi 18 mwanzoni mwa Januari na kuwa mshindani mkuu wa kipa namba moja David De Gea.
Valdes, 33, alikuwa benchi kwenye mechi mbili za mwisho za United. Mchezo wa Ijumaa utakuwa ni mtihani wa kwanza kwake tangu alipoumia goti akiwa na Barcelona miezi 10 iliyopita.
Comments
Post a Comment