VAN GAAL AZIDI KUSHAMBULIWA …AONEKANA KITUKO KWA KUMCHEZESHA DI MARIA KAMA MSHAMBULIAJI, ROONEY KAMA KIUNGO, JONES KUPIGA KONA
Mwandishi Mike Keegan wa Daily Mail, anaongeza idadi ya waandishi na wachambuzi wa soka wanaohoji mbinu za kocha wa Manchester United Louis van Gaal.
Hakuna mchambuzi wa soka nchini England anayekubaliana na mfumo wa 3-5-3 unaotumiwa na Van Gaal na sasa Mike Keegan anashangaa ni vipi kiungo aliyesajiliwa kwa bei mbaya Angel Di Maria achezeshwe kama mshambuliaji.
Mike anasema wakati Di Maria akisajiliwa kwa pauni milioni 59.7, Van Gaal akasema amempata mmoja wa wachezaji bora duniani.
Lakini Di Maria aliyepewa jezi namba 7 iliyotumiwa na wakali kama Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo, bado hatumiki vizuri United.
Mwandishi huyo anashangaa ni vipi Di Maria achezeshwe kama mshambuliji badala ya kiungo wa pembeni halafu hapo hapo unamrudisha mshambuliaji Wayne Rooney akacheze nafasi ya kiungo.
Kama vile hiyo haitoshi, Mike anahoji ni vipi beki Phil Jones anapata nafasi ya kupiga kona mbele ya Rooney, Di Maria na Juan Mata. Van Gaal anajua anachofanya? Anahoji mwandishi huyo.
Mike Keegan alikuwa akichambua mechi ya QPR na Manchester United ambapo alisema kipindi cha pili hususan baada ya Van Gaal kubadili mfumo na kucheza 4-4-2, kilikuwa na msismiko zaidi na hakushangaa United ilipopata magoli mawili na kuchukua pointi tatu muhimu.
Anasema hakubaliani na usemi wa Van Gaal ya kwamba anapochezesha mfumo wa 4-4-2 timu inakosa uwiano.
Aidha mwandishi huyo amewashutumu mabeki Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans kwa kushindwa kufunika mapengo ya Nemanja Vidic, Patrice Evra na Rio Ferdinand.
Comments
Post a Comment