VAN GAAL AMTOLEA UVIVU FALCAO, AMWAMBIA AMTAKA ATHIBITISHE UBORA WAKE …“Kama mchezaji amegharimu pauni milioni 95 au pauni 5,000 kwangu mimi sioni tofauti yoyote”


VAN GAAL AMTOLEA UVIVU FALCAO, AMWAMBIA AMTAKA ATHIBITISHE UBORA WAKE …"Kama mchezaji amegharimu pauni milioni 95 au pauni 5,000 kwangu mimi sioni tofauti yoyote"

Falcao is given a tough welcome to England by Stoke              City defender Marc Wilson at Old Trafford

Kocha Louis van Gaal amesema Radamel Falcao bado anahitaji kuthibitisha ubora wake Manchester United.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa mkopo wa pauni milioni 6 alienguliwa kwenye kikosi cha kwanza na inaaminika alikerwa sana kwa kitendo cha kutochezeshwa kwenye mechi ya kipigo cha 1-0 kutoka kwa Southampton.

Louis van Gaal refused to answer questions about              whether Falcao and Van Persie would start at QPR

Akizungumza kabla safari ya kwenda kuikabili QPR Jumamosi hii, Van Gaal akasema: "Anapaswa kuthibitisha ubora wake. Tumefanya dili na kila kitu kiko wazi. Mwisho wa msimu haujafika, hivyo bado ana nafasi."

"Kama mchezaji amegharimu pauni milioni 95 au pauni 5,000 kwangu mimi sioni tofauti yoyote. Unapaswa kuthibitisha ubora wako."

Aidha, Van Gaal alikataa kuthibitsha kama Falcao atarejea kwenye kikosi kitakachoanza katika mechi dhidi ya QPR.

"Unapaswa kusubiri na kuona nini kitatokea," alisema na kuongeza: "Ninapokiweka hadharani mapema kikosi changu, ninampa wepesi mpinzani wangu."



Comments