UKISHANGAA SARE YA MAN UNITED UTASTAAJABU NA MATOKEO YA CHELSEA NA MAN CITY …zote zafungishwa virago FA Cup, Tottenham na Southapton nazo out
Wakati sare ya 0-0 ya Manchseter United dhidi ya Cambridge United katika michuano ya FA Cup ikizua gumzo kubwa, Chelsea na Manchester City zimetupwa nje baada ya kuchukua vipigo kutoka kwa timu za madaraja ya chini.
Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu imelambwa 4-2 na Bradford City huku Manchester City inayoshika nafasi ya pili ikitupwa nje kwa kufungwa 2-0 na Middlesbrough.
Chelsea iliyokuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumba – Stamford Bridge ikatangulia 2-0 kwa magoli ya Gary Cahill na Ramires lakini kibao kikawageukia na kujikuta wakiaga michuano kwa kupigwa 4-2.
Kulikuwa na matokeo mengine ya kuduwaza Jumamosi hii baada ya Totteham nayo kuaga michuano ya FA kwa kufungwa 2-1 na Leicester City inayoburaza mkia kwenye Ligi Kuu ya England, huku Crystal Palace nayo ikiing'oa Southampton kwa kichapo cha 3-2.
Matokeo ya mechi zote za FA zilizochezwa Jumamosi ni haya hapa. (mechi ya Liverpool na Bolton Wanderers haijajumuishwa).
FT Blackburn Rovers 3 - 1 Swansea City
FT Birmingham City 1 - 2 West Bromwich Albion
FT Cardiff City 1 - 2 Reading
FT Chelsea 2 - 4 Bradford City
FT Derby County 2 - 0 Chesterfield
FT Manchester City 0 - 2 Middlesbrough
FT Preston North End 1 - 1 Sheffield United
FT Southampton 2 - 3 Crystal Palace
FT Sunderland 0 - 0 Fulham
FT Tottenham Hotspur 1 - 2 Leicester City
Comments
Post a Comment