TWANGA PEPETA NAO KUBISHA HODI KIWANJA CHA KIINGILIO KINYWAJI FLAMINGO BAR

TWANGA PEPETA NAO KUBISHA HODI KIWANJA CHA KIINGILIO KINYWAJI FLAMINGO BAR
TWANGA PEPETA NAO KUBISHA HODI KIWANJA CHA KIINGILIO            KINYWAJI FLAMINGO BAR

Bendi ya The African Stars "Twanga Pepeta" Alhamisi hii watakuwa Flamingo Bar Magomeni Mwembechai, kiwanja maarufu kwa show za kiingilio kinywaji chako – yaani kiingilio bure ila usiwe mvivu kuagiza kinywaji.

Hata hivyo show ya Twanga Pepeta kama ilivyokuwa ya FM Academia Jumamosi iliyopita, itakuwa na kiingilio cha shilingi 500o lakini unapewa bia moja bure mlangoni au kinywaji chochote chenye thamani ya iba moja - ni kama 'nusu bure' vile.

Msemaji wa ukumbi huo ameiambia Saluti5 kwa show hizi za viingilio wanazojaribu kuzitambulisha taratibu, zinawalazimisha kufunika sehemu ya wazi ya mbele ya ukumbi kwa magunia ili kudhibiti watu wanaosimama nje ya ukumbi huo wanaoependa kupata burudani ya dezo.

Comments