TUPIA MACHO VIDEO YA DADY DIPIRONE “BADO NAKUPENDA” …ni yule mkali wa masauti aliyeng’ara na Malaika Band



TUPIA MACHO VIDEO YA DADY DIPIRONE "BADO NAKUPENDA" …ni yule mkali wa masauti aliyeng'ara na Malaika Band
TUPIA MACHO VIDEO YA DADY DIPIRONE

Wakati Malaika Band inatambulishwa rasmi mwezi Novemba 2013, mmoja ya watu walioteka hisia za mashabiki ni mwimbaji Dady Dipirone.

Katika wimbo "Nakuhitaji" wakati anatupia sauti yake akisema "Jua nakupenda hata unidangenye mpenzi, jua mapenzi ni mama mayai usiposhikilia vizuri inaweza kuangauka…"  Christian Bella akamtambulisha kama kiongozi wa masauti ya chini. Hakika jamaa ana bonge la 'msauti' anayoweza kuichezea vile atakavyo.

Hakudumu sana Malaika, akatimkia Akudo ambako nako hakukaa sana. Kwasasa ni msanii wa kujitegemea (Solo Artist) na ameachia nyimbo zake kadhaa ambazo zote ni tamu ile mbaya.

Hii hapa ni moja ya kazi zake alizoziachia, ni wimbo unaokwenda kwa jina la "Bado Nakupenda". Itupie macho video yake.



Comments