THEO WALCOTT ASEMA ‘FOWADI’ YA SASA ARSENAL NI BORA KULIKO YOYOTE ILE KATIKA HISTORIA YA KLABU YAO …hata ya kina Thierry Henry na Dennis Bergkamp haifui dafu


THEO WALCOTT ASEMA 'FOWADI' YA SASA ARSENAL NI BORA KULIKO YOYOTE ILE KATIKA HISTORIA YA KLABU YAO …hata ya kina Thierry Henry na Dennis Bergkamp haifui dafu

Theo Walcott in action for Arsenal during their FA Cup              win ove Hull at the beginning of this month

Theo Walcott anaamini safu ya ushambuliaji ya Arsenal ya msimu huu inaweza kuwa kali kuliko yoyote ile katika historia ya timu yao – lakini wanapaswa kuthibitisha hilo kwa kutwaa mataji.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikosa sehemu kubwa ya mwaka 2014 kutokana na kuwa majeruhi, anaamini fowadi ya sasa inayowajumuisha Alexis Sanchez, Olivier Giroud, Santi Cazorla na Alex Oxlade-Chamberlain, itaipiku ile ya kina Thierry Henry na Dennis Bergkamp.

Thierry Henry (right) and Dennis Bergkamp embrace after              the former scored his 100th goal for the Gunners against              Birmingham 

Thierry Henry na Dennis Bergkamp enzi zao

"Wakati nakuja hapa niliwakuta Pires, Ljungberg, Bergkamp, Thierry na Reyes ambao walikuwa moto wa kuotea mbali.

"Lakini nadhani hii ya sasa ni kali zaidi ila tunatakiwa kuthibitisha kwanza," alisema Walcott.



Comments