Habari hii fupi iliyoandamana na picha ya wasanii wa Msondo Ngoma iliandikwa na Saluti5 Septemba 7, 2013 ikiwa na maneno yafuatayo: "HII ni picha iliyopigwa zaidi ya miaka 8 iliyopita, lakini ukiitazama leo hii picha hii inaongea mambo mengi.
Hawa ni wanamuziki wa Msondo Ngoma Music Band, tazama kazi ya mungu ilivyo wasanii wanne waliojipanga kutoka kulia wote ni marehemu. Kulia kabisa ni Joseph Maina, TX Moshi William, Athuman Momba na Ismail Mapanga. Maskini ni kama vile walijua wakajipanga vile.
Anayefuta katika picha baada ya Ismail Mapanga ni Mzee Ali Rashid mwana Zanzibar mmoja wa wapuliza saxophone mahiri kutokea hapa nchini ambaye kwa sasa yupo hoi kitandani akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu." Habari ikaishia hapo.
Lakini kazi ya Mungu juu ya picha hiyo ikaendelea tena mwezi Oktoba mwaka jana ambapo mwanamuziki Ali Rashid mwana Zanzibar alifariki dunia na kufanya wanamuziki watano waliojipanga kwa kufuatana kutoka kushoto mwa picha hii (waliosimama) wote wawe wametangulia mbele ya haki.
Mungu awaweke sehemu inayostahili.
Comments
Post a Comment