MSHAMBULIAJI wa            Liverpool,  Daniel Sturridge anaweza kurudi uwanjani kesho            kuivaa Chelsea katika mechi ya marudiano ya nusu fainali ya            kombe la ligi itayopigwa uwanja wa Stamford Bridge ikitokea            katika majeruhi ya muda mrefu, amesema kocha Brendan Rodgers.
        Nyota huyo wa zamani wa            Chelsea, Sturridge ambaye aliifungia Liverpool magoli 25            kwenye mashindano yote msimu uliopita hajaingia uwanjani tangu            mwezi wa nane mwaka jana kufuatia kupata majeruhi.
        Sturridge alikwenda            Marekani wakati wa Krismas kupata matibabu na aliporudi            alianza mazoezi,na Rodgers anatumaini kumuona mshambulizi huyo            wa England akiwakabilia Chelsea.
        "Amefanya mazoezi vizuri,            sana jana (Sturridge) na ameonekana kuimarika", Rodgers            amewaambia waandishi wa habari.
        
Comments
Post a Comment