Eljero Elia ambaye amejiunga na Southampton kwa mkopo wiki chache zilizopita, ameibuka shujaa kwa timu hiyo baada ya kuifungia magoli mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Newcastle.
Magoli ya Elia yalikuja katika dakika ya 14 na 62 na kuisadia Southampton iendelee kuwa kung'ang'ania nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England nyuma ya Chelsea na Manchester City.
Matokeo ya mechi zote za Ligi Kuu ya Engaland zilizochezwa Jumamosi ni:
Aston Villa0 - 2 Liverpool
Burnley 2 - 3 Crystal Palace
Leicester City 0 - 1 Stoke City
Queens Park Rangers 0 - 2 Manchester United
Swansea City 0 - 5 Chelsea
Tottenham Hotspur 2 - 1 Sunderland
Newcastle United 1 - 2 Southampton
Comments
Post a Comment