SIMBA YATANDIKWA 2-1 NA MBEYA CITY, CHOLO AKOSA PENALTI


SIMBA YATANDIKWA 2-1 NA MBEYA CITY, CHOLO AKOSA PENALTI

mbeyacityfc 1-4 vipers fc_2014_1

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamekubali kichapo cha mabao 2-0  dhidi ya Wagonga Nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Hamad Kibopile na Yusuph Abdallah aliyefunga kwa njia ya penalti, wakati la Simba limefungwa na Ibrahim Hajib 'Mido'.

Hata hivyo dakika ya mwisho ya mchezo, Masoud Nassor 'Cholo' amekosa mkwaju wa penalti baada ya beki Yusuph kumfanyia madhambi Jonas Mkude katika eneo la hatari.

Hiki ni kipigo cha pili kwa Simba ndani ya uwanja wa Taifa, kwani desemba 26 mwaka jana walifungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.



Comments