SIMBA MABINGWA MAPINDUZI CUP 2015 …waitungua Mtibwa kwa matuta, Ivo Mapunda Shujaa wa ghafla

SIMBA MABINGWA MAPINDUZI CUP 2015 …waitungua Mtibwa kwa matuta, Ivo Mapunda Shujaa wa ghafla
SIMBA MABINGWA MAPINDUZI CUP 2015 …waitungua Mtibwa kwa            matuta, Ivo Mapunda Shujaa wa ghafla

Simba SC ya Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kufunga Mtibwa ya Turiani, Morogoro kwa mikwaju ya penalti katika mchezo mkali uliofanyika Uwanja wa Aman, Zanzibar.

Hatua hiyo ya mikwaju ya penalti ilikuwa baada ya timu hizo kutoshana nguvu 0-0 katika dakika 90 za kawaida ambapo kwa mujibu wa taratibu za michuano hiyo, hakuna dakika 30 za nyongeza iwapo timu zitatoka sare.

Simba ilipata penalti nne huku Mtibwa ikipata penalti 3, kila kipa akipangua mkwaju mmoja, wakati penalti nyingine ya Mtibwa ikigonga mwamba.

Kipa Ivo Mapunda wa Simba aliyeingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya mlinda mlango kinda Manyika Peter, ndiye aliyeibuka shujaa baada ya kupangua penalti ya mwisho ya Mtibwa iliyopigwa na Vicent Barnabas.

Comments