Kinda wa Norway Martin Odegaard aliingizwa moja kwa moja kwenye kikosi cha wakubwa katika siku yake ya kwanza ya mazoezi ya Real Madrid aliyojiunga nayo hivi karibuni.
Dogo huyo wa miaka 16 mwenye kipaji cha hali ya juu cha kutandaza soka, alionekana pichani akiwa sambamba na Gareth Bale katika zoezi la kukimbia Alhamisi asubuhi kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Bale alionekana akimhenyesha Odegaard kabla ya baadae kumpa maneno ya kumjenga huku akimkumbatia begeni.
Odegaard anategemewa kumalizia sehemu ya msimu iliyobakia akiwa na timu B lakini siku zote atakuwa akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza chini ya kocha Ancelotti.
Comments
Post a Comment