SIKU KHADIJA YUSSUF NA FATMA MCHARUKO WALIPOKARIBISHWA STUDIO ZA PILI PILI FM MOMBASA



SIKU KHADIJA YUSSUF NA FATMA MCHARUKO WALIPOKARIBISHWA STUDIO ZA PILI PILI FM MOMBASA
SIKU KHADIJA YUSSUF NA FATMA MCHARUKO WALIPOKARIBISHWA              STUDIO ZA PILI PILI FM MOMBASA

Mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana, waimbaji nyota wa Jahazi Modern Taarab, Khadija Yussuf na Fatma Mohamed "Mcharuko" walikaribishwa studio za Pili Pili FM ya mjini Mombasa na kufanya mahojiano mafupi.

Fatma Mcharuko au Fatma Nyoro kama anavyojiita sasa hivi pamoja na Khadija Yussuf walifanya mahojiano na mtangazaji Aisha Abushiry maarufu kama Mamaa Madikoko kupitia kipindi cha kila siku cha Chachandu za Taarab.

Mamaa Madikodiko ameiambia Saluti5 kuwa kama kuna siku ambayo alipokea meseji nyingi kwenye kipindi chake basi siku aliyowahiji Khadija na Mcharuko ni moja siku zilizopata meseji kibao kutoka kwa wasikilizaji wao.

Mcharuko na Khadija walikuwa Mombasa kwaajili ya tamasha kubwa Usiku wa Mirindimo lililofanyika mjini humo.

 Khadija Yussuf (kushoto) na Fatma Mcharuko (kulia) wakiwa na Mamaa Madikidiko

 Khadija Yussuf, Mamaa Madikidiko na Fatma Mcharuko 

  Khadija Yussuf, Mamaa Madikidiko na Fatma Mcharuko katika picha ya pamoja

 Khadija Yussuf akiwa katikati ya mahojiano

 

Mamaa Madikoko akisoma meseji za wasikilizaji

 





Comments