RONALDO SASA AWA WA TATU ORODHA YA WAFUNGAJI WA MUDA WOTE MADRID


RONALDO SASA AWA WA TATU ORODHA YA WAFUNGAJI WA MUDA WOTE MADRID

image-1-for-paper-pics-02-jan-2011-gallery-502540023

Baada ya kufunga goli mbili jana, Nyota na mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2014, Cristiano Ronaldo ameefanikiwa kumpiku Carlos Alonso Santillana na hatimaye kuwa wa tatu katika orodha ya wafungaji wa muda wote wa klabu hiyo kunako michuano mbalimbali. Ronaldo amefikisha magoli 289 akimwacha Santillana mwenye 288.

katika idadi hiyo mabao 206 ameyafunga katika ligi, mabao 21 kunako kombe la mfalme, mabaoo 57 katika michuano ya klabu bingwa ulaya, mawili michuano baina ya bingwa wa UEFA kubwa na ndogo na mengine matatu katika pambano la ufunguzi wa ligi ya Hispania.

na kwa maana hiyo sasa, Ronaldo, almaarufu CR7 amebakiza magwiji wawili pekee ambao ni Alfredo Di Stéfano mwenye 307 na mhispaniola Raúl González, mwenye 323.



Comments