ROMA YAWATENGEA MANCHESTER UNITED KEVIN STROOTMAN …yasema haimuuzi lakini kija ofa ya maana biashara ipo
Rais wa Roma James Pallotta amefichua kuwa hana mpango wa kumuuza kiungo wake nyota Kevin Strootman, lakini akakiri kuwa kama itakuja ofa nono basi klabu italazimika kusikiliza.
Manchester United wamekuwa wakihusishwa na ada ya pauni milioni 32 kwa Strootman, ambaye tetesi zilizagaa sana kuwa anaondoka Roma licha kusaini mkataba mpya wa miaka mitano mwaka 2013.
Pallotta ameiambia Bleacher Report: "Maoni yangu ni kwamba sitaki Kevin aondoke, lakini kama mtu atakuja na ofa ya maana, unapaswa kusikiliza.
Unaendesha timu, hivyo unapaswa kuangalia kipi ni bora zaidi kwa kila mmoja na sio kuangalia kwa ubinafsi. Hivyo ndiyo ulimwengu huu unavyokwenda".
Louis van Gaal ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo ambaye alimfundisha wakati akiikochi timu ya taifa ya Holland.
Comments
Post a Comment