Paris Saint-Germain (PSG) imeichapa Evian 4-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa na kusogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligue 1.
Ulikuwa ni ushindi wa kufa na kupona kwa PSG ambayo inaendelea kubaki nyuma kwa pointi nne kwa vinara wa ligi hiyo Olympique Lyonnais iliyoichapa RC Lens 2-0 Jumamosi.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa PSG ndani ya mechi zake nne za mwisho, shukurani kubwa ziwaendee Pastore na Cavani waliofunga magoli ya ushindi.
Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Cedric Barbosa alifunga bao tamu la kuongoza kwa Evian dakika ya 14 lakini beki wa zamani wa Chelsea David Luiz akaisawazishia PSG dakika 15 baadae.
Marco Verratti akapatia PSG bao la pili dakika ya 38, goli lililodumu hadi dakika ya 63 wakati Gregory van der Wiel alipojifunga na kufanya mambo yawe 2-2.
Kiungo wa Kiargentina Javier Pastore akawafungia mabingwa watetezi goli la tatu kunako dakika ya 74 huku Edinson Cavani akihitimisha ushindi kwa kupachika bao la nne dakika moja kabla ya mpira kumalizika.
Comments
Post a Comment