Mchezaji mkongwe wa Juventus, Andrea Pirlo ameitaka Manchester United isahau suala la kumsaliji tena Paul Pogba na kuwaambia waendelee kula maumivu ya makosa waliyofanya ya kumruhusu mchezaji huyo aondoke Old Trafford.
Hatma ya kiungo huyo wa Kifaransa imekuwa gumzo kubwa barani Ulaya kwa miezi sita iliyopita na vita kwa kumsajili ndio kwanza vinatarajiwa kupamba moto.
Louis van Gaal ni mmoja kati ya watu wanaovutiwa na Pobga ambaye bei yake inaweza kufika pauni milioni 70.
Lakini Pirlo amesisitiza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 hatarejea Old Trafford ambako alinyimwa nafasi ya kuonyesha uwezo wake chini ya kocha wa zamani Sir Alex Ferguson.
"Kwasababu zozote zilizowafanya washindwe kumpa nafasi – ni makosa ambayo wanastahili kuendelea kula maumivu yake," alisema Pirlo na kuongeza: "Sioni kama uwezekano wa Pobga kurejea Manchester United."
Comments
Post a Comment