Picha za Samatta katika majaribio CSKA Moscow na listi ya vilabu vingine vinavyomtaka


Picha za Samatta katika majaribio CSKA Moscow na listi ya vilabu vingine vinavyomtaka

15922_870694186307442_880608052995095050_nHatimaye nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta imeanza kung'ara katika anga ya kimataifa ya soka.

Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mshambuliaji huyo yupo kwenye majaribio katika klabu ya CSKA Moscow – moja ya klabu kubwa kabisa nchini Urusi ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo na kucheza katika michuano ya mabingwa wa ulaya.

10690055_930864356931841_364362052221467735_n

Samatta alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku 3 na klabu hiyo kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini sasa ameongezewa wiki moja ya ziada ili maofisa ya jopo ya ufundi la timu hiyo wapate muda wa kumuangalia vizuri.

10689498_930864360265174_71847191900962169_n

Pamoja na CSKA Moscow – timu nyingine ambazo zinatajwa kumtaka mshambuliaji huyo ni Inter Milan na Udinese za Italia, Atletico Madrid ya Spain, FC Basel ya Uswis na Kaiserslauten ya Ujerumani.



Comments