Paul Pogba amefungua milango ya kurejea Manchester United baada ya kufichua kuwa bado anaipenda timu hiyo aliyoiacha mwaka 2012 na kujiunga na Juventus.
Huku vilabu vikubwa barani Ulaya vikipiga hesabu ya kwenda kwa vinara wa Serie A kusaka saini ya kiungo huyo wa Kifaransa, Pobga amesema ana biashara ya ambayo haikukamilika Old Trafford na kusema hana hisia mbaya baada ya kuondoka bure baada ya kukosa nafasi ya kikosi cha kwanza.
"Nina papara," alisema Pobga katika maongezi yake na jarida la FourFourTwo alipozungumzia kuondoka kwake United.
"Ilikuwa ni hisia zangu. Kocha (Sir Alex Ferguson) aliniamini lakini hakunipa nafasi. Alisema nilikuwa bado kijana sana.
"Aliniambia 'muda wako utafika' lakini haikuwa hivyo. Lakini haimaanishi kuwa nitaiongelea vibaya United. Naipenda klabu."
Comments
Post a Comment