PANAMA FC, BOOM FC KUANIKA 18 BORA LIGI YA MKOA WA DAR ES SALAAM … LIGI YA WANAWAKE NAYO KUANZA MWEZI UJAO
Mechi ya kiporo katika michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam kati ya klabu za Panama FC dhidi ya Boom FC, itapigwa Jumanne kwenye uwanja wa Airwing,ukiwa ni mchezo ambao utatoa fursa kwa DRFA kutangaza timu 18 zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya 18 bora ya michuano hiyo.
Michuano hiyo ya ligi mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,inaingia katika hatua ya mwisho katika hatua ya mwisho ambayo itatoa wawakilishi wa mkoa Dar es salaam katika ligi ya mabingwa wa mikoa ya TFF.
Kivumbi cha hatua ya 18 bora,kitaanza kutimka tarehe 4 /02/2015.
Wakati huo huo, Ligi ya soka la wanawake kwa mkoa wa Dar es salaam inataraji kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao kwa kushirikisha jumla ya timu 12,zitakazoumana kuwania ubingwa huo.
Itakumbukwa kwamba DRFA iliamua kusogeza mbele mashindano hayo ambayo yalikuwa yaanze januari 16/2015,kutokana na upungufu wa wachezaji kwa timu husika ambao wengi wao wanashiriki mashindano ya kuwania kombe la Taifa Wanawake,ambayo sasa imeingia katika hatua ya robo fainali.
Timu zote 12 zitakazoshiriki ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam,zitawekwa hadharani hapo baadaye.
IMETOLEWA NA AFISA HABARI DRFA
Omary Katanga
Comments
Post a Comment