NI FAINALI YA WATOTO WA LONDON, TOTTENHAM YAIFUATA CHELSEA WEMBLEY CAPITAL ONE CUP …Christian Eriksen mwiba mkali kwa Sheffield United
Kama Chelsea walikuwa na njozi za kupata mchekea kwenye fainali ya Capital One Cup, basi njozi hizo zimeyeyuka - watoto wenzao wa London Tottenham ndiyo waliopenya kwenda Wembley baada ya kuitoa Sheffield United kwa jumla ya mabao 3-2.
Tottenham ililazimishwa sare ya 2-2 na Sheffield United Jumatano usiku lakini faida ya ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza ikawavusha kwenda fainali itakayopigwa mwezi Machi.
Hata hivyo safari ya Totteham kwenda fainali haikuja kirahisi, ilikuwa ni mechi ya mshike mshike ambapo bao lao la dakika ya 28 kupitia kwa Christian Eriksen, likarudishwa dakika ya 77 na Che Adams shabiki wa utotoni wa Arsenal ambaye dakika mbili baadae akatupia tena goli la pili na kufanya Tottenham iwe nyuma 2-1.
Wakati Sheffield United wakipambana kusaka bao la tatu ambalo lingewapa tiketi ya Wembley, Christian Eriksen akaibuka shujaa kwa kuisawazishia Tottenham dakika ya 88.
Chelsea ilitangulia fainali siku ya Jumanne baada ya kuifunga Liverpool 1-0 na kuvuka kwa jumla ya bao 2-1.
Sheffield United (4-1-4-1): Howard 7; Flynn 7, Basham 6, McEveley 6, Harris 6; Doyle 5 (Reed 65, 6); Campbell-Ryce 5 (Adams 7.5), Baxter 5, Scougall 5, Murphy 6; McNulty 5 (Higdon)
Tottenham (4-2-3-1): Vorm 6; Walker 6, Dier 6, Vertonghen 6, Davies 6; Stambouli 7, Mason 7; Lamela 6 (Townsend), Erisken 8, Dembele 6.5 (Paulinho 65, 6); Kane 7.5.
Comments
Post a Comment