Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya, Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni, ambayo pia hujulikana kama viumbe wa ajabu Anunnaki Alien. Bendi hii inayoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja imejikuta ipo katika hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa kutumbuiza maonyesho zaidi katika msimu ujao wa joto (Summer). Watayarishaji wa maonyesho makubwa ya nje barani Ulaya wanashinikizwa na washabiki wao lazima waipandishe jukwaani Ngoma Africa Band kutokana na mdundo wao Bongo dansi, mapromota hao baada kuwekwa roho juu na washabiki wao, nao wamedhamiria kuwapambanisha washabiki hao na bendi maarufu Ngoma Africa band yenye makao yake nchini Ujerumani. Habari za uhakika zimetonya kuwa bendi hiyo imekubali kuenda kutumbuiza katika nchi za Latvia na Austria na maonyesho mengine katika msimu wa joto, pia taarifa zinasema kuwa hali hiyo ya tabia za washabiki kushinikiza maonyesho inaifanya bendi ya Ngoma Africa band kuwa katika mzunguko wa maonyesho makubwa na wanamuziki kukosa muda wa kupumzika.Lakini hakuna ubishi kuwa kamanda Ras Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina yake wa kuwamudu washabiki wao kule barani Ulaya. FFU-ughaibuni pia wanasikika online at www.ngoma-africa.com
Comments
Post a Comment