Barcelona imetinga nusu fainani ya Copa del Rey baada ya kuifunga Atletico Madrid 3-2 na kuvuka kwa jumla ya bao 4-2, shukran nyingi zinakwenda kwa mshambuliaji wa Brazli Neymar aliyefunga mabao mawili.
Fernando Torres mchezaji wa zamani wa Chelsea, anaonyesha dhahir 'kukufuka' upya kwenye timu yake ya utotoni ambapo ilimchukua sekunde 39 tu kuipatia Atletico bao la kuongoza.
Hata hivyo, dakika 9 baadae Neymar akaisawazishia Barcelona baada kupokea 'pande' tamu kutoka kwa Luis Suarez kabla ya Raul Garcia kufungia Atletico Madrid bao la pili dakika ya 30 kwa penalti ya utata.
Beki wa kutumainiwa wa Atletico Miranda akajifunga dakika ya 38 huku Neymar akihitimisha funga nikufunge kwa kuipa Barcelona bao la ushindi dakika nne kabla ya mapumziko kufuatia kazi nzuri iliyofanywa Lionel Messi.
ATLETICO MADRID (4-4-2): Oblak; Juanfran (Gamez, 58), Giménez de Vargas, Miranda, Siqueira; Raul Garcia, Gabi, Suárez, Turan (Cani, 63), Griezmann (Ñíguez, 45); Torres
Booked: Raul Garcia, Gabi sent off, Turan
BARCELONA (4-3-3): Ter Stegen; Dani Alves, Pique, Mascherano (Mathieu 61), Alba; Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suarez, Neymar (Pedro, 77)
Comments
Post a Comment