MUNGU ASHUKURIWE KWA KUNILETA ARSENAL, ASEMA BEKI MPYA GABRIEL PAULISTA …asema mambo mazuri yanakuna Emirates


MUNGU ASHUKURIWE KWA KUNILETA ARSENAL, ASEMA BEKI MPYA GABRIEL PAULISTA …asema mambo mazuri yanakuna Emirates

Gabriel Paulista poses with an Arsenal shirt as the              club unveil their new signing on Wednesday

Beki kisiki kutoka Villarreal Gabriel Paulista ameonyesha furaha isiyo kifani kupata nafasi ya kucheza Premier League na kusema njozi yake ya kujiunga na Arsenal imekuwa kweli.

Mchezaji huyo mzaliwa wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 alipata hati ya kufanya kazi England licha ya kutoichezea timu yake ya taifa hata mechi moja na hivyo kukamilisha usajili wake wa pauni 11.2 kwa mkataba wa miaka minne.

"Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii," Gabriel Paulista aliiambia website ya Arsenal. "Shukran kwa Mungu, klabu hii ya kipekee kuja kwangu na kuhitaji huduma yangu, kuona kuwa ninaweza kuwasaidia ni jambo la kusisimua sana.

"Sitawaangusha, nitajitolea kwa uwezo wangu wote na hakika mambo mazuri yanakuja."



Comments