MTOTO WA RONALDO MATATA SANA, ATEKA VICHWA VYA HABARI KAMA BABA YAKE …afanya kituko cha kukatisha mahojiano ya baba
Mtoto wa Cristiano Ronaldo kwa wiki nzima amekuwa akiteka vichwa vya habari kama baba yake – na habari iliyotesa zaidi ni ile ya mtoto huyo wa miaka minne kuzamia kwenye mahojiano ya baba yake huku akiwa kavalia kama Superman.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alikuwa akihojiwa na channel rasmi ya timu ya taifa ua Ureno baada ya kushinda tuzo ya Ballon d'Or Jumatatu.
Mwanae, Cristiano Jnr aliyekuwa chumba kingine akavamia na vazi lake la Superman na kukatisha kwa muda mahojiano na kupelekea kicheko kwa baba yake.
Cristiano Jnr akidekezwa kidogo na mtangazaji
Ronaldo anamkumbatia mwanae huku akiendelea na mahojiano
Hapa anamnong'oneza mwaneye
Comments
Post a Comment