MSAFIRI DIOUF MATAWI YA JUU …YUKO MAPUMZIKONI UINGEREZA

MSAFIRI DIOUF MATAWI YA JUU …YUKO MAPUMZIKONI UINGEREZA
MSAFIRI DIOUF MATAWI YA JUU …YUKO MAPUMZIKONI UINGEREZA

Rapa na mwimbaji wa Twanga Pepeta mwenye kipaji cha hali ya juu, Msafiri Diouf yuko nchini England kwa ziara ya kifamilia zaidi.

Msanii huyo ambaye tangu arejee Twanga Pepeta, ametunga nyimbo mbili ukiwemo "X-Michepuko" atakuwa huko kwa wiki kadhaa.

Meneja wa Aset inayomiliki Twanga Pepeta, Hassan Rehani aliithibitishia Saluti5 kuwa ni kweli Diouf yupo England na safari hiyo imepewa baraka zote na bendi.

"Aliomba likizo fupi kwaajili ya kwenda kujipumzisha huko, ni safari ya kifamilia zaidi," alisema Hassan Rehani.

Comments