MOURINHO ANATAKA CHELSEA YA AINA GANI? APELEKA OFA KUMNASA DOUGLAS COSTA LAKINI YAPIGWA CHINI … Douglas Costa mwenyewe asema hajakata tamaa
Licha Chelsea kuwa mbele kwa pointi tano katika Ligi Kuu ya England huku timu ikionekena kukamilika kila idara, kocha Jose Mourinho bado anataka kufanya usajili wa kishindo dirisha hili la Januari.
Chelsea ikapeleka ofa ya pauni milioni 16 kumsajili kiungo bab kubwa wa Shakhtar Donetsk, Douglas Costa lakini ofa hiyo ikapigwa chini.
Kwa mujibu wa Douglas Costa raia wa Brazil umri wa miaka 24, ni kwamba iwapo usajili huo utakamilika basi utakuwa ni uhamisho wa ndoto yake.
Akizungumza na vyombo vya habari katika ziara ya timu yake huko Amerika ya Kusini, Costa alisema ofa Chelsea imekataliwa – lakini atajaribu kuongea na klabu yake ili kushinikiza uhamisho huo.
""Ni njozi kuichezea Chelsea, nafasi ya kipekee. Nitajaribu kuongea na uongozi, Costa aliliambia gazeti la Globo Esporte la Brazil.
Shakhtar Donetsk haipo tayari kumwachia mmoja wa wachezaji wake nguzo kwa bei ya kutupa.
Comments
Post a Comment