Dunia ina mengi ya kuyakumbuka kuhusu bondia Mike Gerard            Tyson, kuna ile rekodi ya kushinda mapambano mengi, makubwa            lakini umri wake ulikuwa mdogo tu!
        Aliweza kutengeneza umaarufu mkubwa, pesa nyingi kwenye            umri mdogo na pia dunia ilikuwa na mtandao mdogo wa habari            lakini kila mtu alimfahamu wakati ule.
        Mike Tyson kajaribu na upande huu, kashirikishwa na collabo            na staa Madonna, inaitwa ' iconic' ambayo ni moja ya            nyimbo ambazo ziko katika album ya Madonna, Rebel Heartambayo            iliibiwa na kuuzwa mtandaoni mwaka 2014 mwishoni na jamaa            mmoja raia wa Israel.
        "Sikujua kama Madonna aliniita pale kwa ajili ya kupiga              story au kurap… niliongea kuhusu maisha yangu na nilisema              mambo ambayo yaliwahi kuniumiza … " Tyson akiongelea            namna walivyofanya collabo hiyo.Sauti yake imesikika mwanzoni            kama mtu anayerap, sauti yake imefanyiwa utaalamu wa computer            hivyo haisikiki kama sauti yake halisi.Hapa unaweza            kuisikiliza collabo hiyo.
        
Comments
Post a Comment