MESSI ASEMA KUBALI USIKUBALI JOSE MOURINHO NI KOCHA BORA …Je anapalilia njia ya kwenda Chelsea?



MESSI ASEMA KUBALI USIKUBALI JOSE MOURINHO NI KOCHA BORA …Je anapalilia njia ya kwenda Chelsea?

Messi has cast doubt over his Barcelona future,                admitting 'I don't know where I'll be next year'

Supastaa wa Barcelona Lionel Messi ameendelea kuacha maswali mengi baada ya kumimina sifa kwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho na kusema kuwa kwa sasa huyo ndiye kocha bora.

Kumekuwa na uvumi mkubwa wa Messi kutimkia Chelsea au Manchester City na hali imezidi kuwa tata baada ya nyota huyo kusema hajui ataitumikia timu gani msimu ujao.

Kwa kusema hivyo, Messi amemaanisha kuwa licha ya siku zote kusema anatamani kumalizia soka yake Barcelona lakini sasa hana ukakika tena na jambo hilo.

Katika kura yake aliyopiga kwenye tuzo za FIFA Ballon d'Or, Messi akamchagua Mourinho kama kocha bora wa mwaka na kumnyima kura kocha wake wa timu ya taifa Alejandro Sabella ambaye alistaafu mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka uliopita.

Messi pia alimyima kura kocha wake wa zamani katika Barcelona Pep Guardiola.

Messi anasema "Mourinho ni kocha bora, iwe unampenda au humpendi, ni lazima ukubali kuwa ni kocha bora duniani."

Je kauli hiyo inamaanisha kuwa siku moja Messi angependa kucheza chini ya Mourinho? Ni suala la kusubiri.



Comments