Jumapili usiku Lionel Messi alifunga 'hat-trick' (magoli matatu katika mechi moja) yake ya 30 kwa Barcelona na ya 22 katika La Liga pale aliposaidia timu yake kuingamiza Deportivo la Coruna 4-0.
Magoli hayo matatu yanamfanya Messi awe mchezaji wa pili kupiga 'hat-trick' 30 kwa timu za Hispania baada ya Telmo Zarra.
Hiyo pia inamfanya Messi awe amefunga magoli 19 katika mechi 19 huku Barcelona ikiifikia nusu ya msimu wa La Liga ikiwa katika kiwango cha hali ya juu.
Messi alifunga katika dakika ya 10, 33 na 62 huku Sidney akijifunga dakika ya 83 na kuizawaia Barcelona bao la nne.
Kwa kiwango anachoendelea kukionyesha Messi, ni wazi kuwa anataka kuhakikisha anashinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia mwakani, tuzo ambayo inashikiliwa na mpinzani mwake mkubwa Cristiano Ronaldo kwa mwaka wa pili mfululizo.
Comments
Post a Comment