MBUNGE WA SIKONGE SAID NKUMBA ALIVYOTESA JUKWAA LA MSONDO LEADERS CLUB …pata picha 15 za onyesho hilo
Mbunge wa jimbo la Sikonge Mheshimiwa Said Nkumba Ijumaa usiku aliliteka onyesho la Msondo Ngoma pale Leaders Club baada ya kuonyesha umahiri wa kuimba nyimbo za bendi hiyo.
Lakini si hivyo tu, Said Nkumba akaonyesha pia umahiri wa kulicheza Msondo, kila aina ya uchezaji wa Msondo alikuwa nao kichwani.
Ukiondoa burudani ya Mheheshimiwa Nkumba, Msondo Ngoma nao kama kawaida yao huwa hawaribu, waliachia show maridadi.
Tupia macho baadhi ya picha zake pamoja na picha za baadhi ya wasanii wa Msondo Ngoma.
Mheshimiwa Said Nkumba (kulia) akisakata Msondo
Goma la Msondo linaendelea kukolea
Msanii wa filamu Seif Mbembe (kushoto) akicheza na Mheshimiwa
Said Nkumba na Mbembe wakiendelea kula rumba
Hapa sasa Mheshimiwa Said Nkumba yupo kwenye uimbaji
Said Nkumba aikiimba kea usahihi moja ya nyimbo za Msondo
Athuman Kambi akiimba na Said Nkumba
Mwimbaj Juma Katundu akicheza Slyia Mwakilufi Shemejiiiii
Huu sasa ni mduara wa mashabiki wa Msondo
Waimbaji Twanha, Kambi na Katundu wakishambulia jukwaa
Abdul Ridhwan Pangamawe akifurahia kazi yake
Mnyupe na Romario na ala zao za upepo
Mwimbaji Twaha Malovee
Hassan Moshi TX Jr
Huyu ni Kidevu cheupe Zahoro Bangwe akifanya yake
Comments
Post a Comment