Mats Hummels amewaambia Borussia Dortmund kwamba uaminifu wake kwa klabu hakuzuii uwezekano wa yeye kujiunga na Manchester United.
United inamtaka Hummels ili kuimarisha safu yake ya ulinzi iliyopwaya na wako tayari kulipa pauni milioni 30 kumnasa sentahafu huyo aliyeng'ara na Ujerumani katika Kombe la Dunia iwapo ataamua kuondoka Dortmund.
Hummels, 26, mchezaji wa zamani wa Bayern Munich ametoa ishara kuwa si rahisi kwake kujiunga na kikosi cha Louis van Gaal katika dirisha hili la usajili, lakini ameacha milango wazi kwa safari ya kwenda Old Trafford.
Beki huyo ameionya Borussia Dortmund kuwa utiifu wake kwa klabu haumzuii kwenda Manchester United.
"Nitasimama katika njia yangu ya kutoahidi chochote na pengine siku moja nitaondoka, badala ya kusema nitakaa milele halafu baadae niondoke ghafla," alisema Hummels.
Comments
Post a Comment