GHANA, 'Black Stars' imeitungua Algeria 1-0 katika mechi ya pili yakundi C ya michuano ya mataifa ya Afrika iliyopigwa uwanja wa Estadio de Mongomo.
Nahodha Asamoah Gyan alirejea uwanjani baada ya kusumbuliwa na malaria, ameifungia Ghana bao la ushindi katika dakika ya 90.
Ushindi huo umewafanya Ghana waungane na Senegal inayocheza muda huu, Algeria na Senegal katika idadi ya pointi tatu.
Comments
Post a Comment