MASHUJAA BAND WAVAMIA ANGA ZA SKYLIGHT BAND …sasa ni ndani ya Thai Village kila Jumapili

MASHUJAA BAND WAVAMIA ANGA ZA SKYLIGHT BAND …sasa ni ndani ya Thai Village kila Jumapili
MASHUJAA BAND WAVAMIA ANGA ZA SKYLIGHT BAND …sasa ni            ndani ya Thai Village kila Jumapili

Bendi bora ya muziki wa dansi Tanzania, Mashujaa Band kuanzia Jumapili hii na kila Jumapili watakuwa wakipatikana ndani ya Thai Village Masaki.

Meneja masoko wa Mashujaa Maxi Luhanga, ameiambia Saluti5 kuwa maandalizi yote ya bendi yao kuanza kutumbuiza Thai Village yamekamilika.

Thai Village ndio ngome ya Skylight Band ambayo hupiga hapo kila Ijumaa na kuongezeka kwa Mashujaa kunamaanisha kuwa kiwanja hicho sasa kinaanza kuwa na mvuto kwa bendi zingine.

Comments