MARTIN KEOWN ASEMA SUAREZ NI BORA KULIKO DIEGO COSTA


MARTIN KEOWN ASEMA SUAREZ NI BORA KULIKO DIEGO COSTA

Martin Keown reveals he would rather have Suarez in                his team than Chelsea striker Costa

Beki wa zamani wa Arsenal Martin Keown amesema Luis Suarez ni bora zaidi kuliko Diego Costa na kwamba mshambuliaji huyo wa Barcelona angefunga magoli mengi zaidi Chelsea kuliko Costa.

Diego Costa ameingia kwa kishindo Premier League tangu alipojiunga na Chelsea kutoka kwa mabingwa wa La Liga Atletico Madrid kiangazi kilichopita kwa pauni milioni 32.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania mzaliwa wa Brazil, anaongoza chati ya ufungaji akiwa ameshatupia wavuni mabao 17 katika msimu wake wa kwanza England.

Costa has taken the Premier League by storm during his              debut season in English football

Suarez bado anasota kukifikia kiwango chake alichokionyesha Liverpool msimu ulipita na kufanya Barcelona imnunue kwa pauni milioni 70. Amefunga magoli matano tu katika mechi 17 alizocheza.

Lakini Keown ambaye anajua ugumu kwa kukabiliana na mshambuliaji wa kiwango cha juu, amebainisha kuwa angependa kuwa na Suarez kwenye timu yake kuliko Costa.

"Nadhani Suarez ni mchezaji bora zaidi. Wakati Costa anaitumikia Hispania kombe la dunia alishindwa kufurukuta, lakini Suarez aliyekuwa anarejea uwanjani baada ya upasuaji wa goti alionyesha ubora wake.

"Kama Suarez angekuwa anaichezea Chelsea basi angefunga magoli mengi zaidi ya haya yaliyofungwa na Costa. Hata hivyo namchukulia Costa kama mshambuliaji wa hali ya juu baada ya mwanzo wake mzuri kwenye Premier League lakini kama wanasoka halisi, nadhani Suarez ni bora kuliko yeye."



Comments