Manchester United imebanwa na timu ndogo ya daraja la pili Cambridge United na kulazimishwa sare ya bila kufungana katika mchezo wa FA Cup – raundi ya nne na sasa timu hizo zitalazimika kurudiana Old Trafford.
Ikiwa na kikosi kilichosheni mastaa wa bei mbaya, United ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini ikapoteza mwelekeo kipindi cha pili kabla ya kucharuka tena mwishoni kabisa mwa mchezo.
Kipa wa Cambridge United Chris Dunn alichomoa michomo michache ya hatari huku mabeki wa kati Michael Nelson na Josh Coulson wakisimama imara dhidi ya washambuliaji wa Manchester United.
Mshambuliaji anayeichezea Manchester United kwa mkopo Radamel Falcao akapiga shuti moja tu lililolenga goli huku Di Maria akijaribu mara mbili.
Kocha wa Manchester United ambaye mfumo wake wa 3-5-2 unalaumiwa sana, alishikwa na ghadhabu akisema uwanja wa Cambridge ni mbovu lakini pia akashutumu waamuzi.
"Ni kweli nimechukia na hii ni sehemu ya kazi yangu. Kila mara kocha unapenda kuwa na furaha lakini vitu vingine vinakuwa nje ya uwezo wako.
"Inaelekea sasa kila mtu yuko dhidi yetu, uamuzi ulikuwa na dosari nyingi," alisema Van Gaal.
Cambridge Utd: Dunn 8, Tait 7, Nelson 8.5, Coulson 7.5, Taylor 7, Champion 7.5, Hughes 6.5 (Chadwick 76), Donaldson 8, McGeehan 6, KaiKai 5.5 (Dunk 53, 6), Elliott 6.
Man Utd: De Gea 6, Valencia 5.5, Jones 6, Rojo 6, Blind 7 (Shaw 86), Carrick 6, Fellaini 5 (Herrera 67, 6), Januzaj 6, Di Maria 6.5, Wilson 5 (van Persie 67, 6), Falcao 5.
Comments
Post a Comment