MALAIKA BAND ‘YASIKILIZA’ KILIO CHA MASHABIKI WAO …kiingilio Mango Garden sasa buku 7 tu


MALAIKA BAND 'YASIKILIZA' KILIO CHA MASHABIKI WAO …kiingilio Mango Garden sasa buku 7 tu
MALAIKA BAND 'YASIKILIZA' KILIO CHA MASHABIKI WAO            …kiingilio Mango Garden sasa buku 7 tu

Kwa kile walichokiita kusikiliza kilio cha mashabiki wao, Malaika Band wamepunguza bei ya kiingilo chao ndani ya Mango Garden kutoka shilingi elfu 10 hadi elfu 7.

 

Kwa maana hiyo, kiingilio cha shilingi elfu 1o kwa Malaika Band hapo Mango Garden kimedumu kwa wiki mbili tu na sasa mashabiki wao wataingia kwa buku saba kama ilivyokuwa zamani.

Malaika Band hupatikana Mango Garden kila Ijumaa na kwa sasa siyo siri kuwa hiyo ndiyo bendi yenye mafanikio makubwa zaidi ndani ya ukumbi huo kuliko bendi zote zinazopiga hapo.

Rais wa bendi hiyo, Christian Bella ameimbia Saluti5 kuwa kwa vile huo ndiyo ukumbi wao wa nyumbani huku mashabiki wengi wakiomba ahueni hususan kwa miezi hii ya mwanzo wa mwaka, basi wameamua kurejesha kiingilio cha zamani hadi hapo baadae.

Bella amesema katika kipindi hiki cha mpito, kama Malaika watakuwa na maonyesho maalum basi kiingilio cha shilingi elfu kumi kitatumika.



Comments