Na Othuman Rolenza
Nimeona niwasilishe mawazo yangu kwenye suala hili ambalo limepelekea hata kuwagawa marafiki wa muda mrefu (J.B na Mtitu John), pia limepekea mpaka serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni kuingia kati na kutolewa kwa taarifa mwishoni mwa mwezi Disemba 2014.
Katika taarifa hiyo WIZARA KUPITA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO ilitoa taarifa ya kuzuia kampuni ya Steps kuuza 'MOVIE ZAKE' KWA BEI YA Tshs 1,000/= KWA MAELEZO KWAMBA ….." Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu.
Upande wa akina Mtitu na wasabazaji wengine wakiwa na kiongozi wa TAFF Ndg, Mwakifamba wao wanahoji kwamba kitendo hiki cha Kampuni ya STEPS ENT. kitapelekea kuwa makapuni mengine madogo kuangauka na mwisho wao kubaki pekee yao wakihodhi soko. William Mtitu alikwenda mbali zaidi na kusema akina RITCHIE ,JB , MZEE MAJUTO na wengine wamepewa pesa kwa ajili ya kulipigipia debe hilo, pia alinukuliwa na gazeti la VIBE wa mwezi NOVEMBER 2014, kwamba hata Mzee majuto yupo kwenye mpango huo ambao kwa tafsiri yake unalengo la kuwaondoa wao kwenye soko.
STEPS ENT. wao nilimsikia BOND BIN SINAN katika kipindi cha Friday Night Live na nilimsikiliza mwakilishi wa steps katika ukumbi wa habari maelezo wote kwa pamoja hoja zao ni kwamba wameshusha bei kupambana na uharamia ambapo kwa sasa CD ya ANORLD SHAWZNIGER , JEAN CLAUDE VAN DAMME INAUZWA Tsh 2000 au 1500 zikiwa collection za movie 20, tena kwa maelezo yake movie hizo zimetengenezwa kwa garama kubwa ikiwepo watu wanapasua vio, wanaruka juu ya magarofa (nadhani anazungumiza technoligia na garama zinazotumika) huku mseamji wa STEPS ENT, yeye alisema kwamba kitendo cha kampuniyake kupunguza bei kimevunja sheria gani, katika kikao hoja yake ya msingi ilikuwa hii, kwamba wao hawajavunja sheria yoyote.
Baada ya kikao hicho ndipo SERIKALI KUPITIA WIZARA HUSIKA itakoa taarifa '….." Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu. (nukuu). Sanjari na hilo waandaji wengine CHIKI MCHOMA, BOND BIN SINAN WASTARA JUMA, JUMMY MAFUFU NA JOHN LISTA wao wamepinga vikao viwili vilivyofanyika kama haviku washirikisha na kuomba wao kama waadndaji wapate nafasi pia, ni hoja zuri ila unaweza kujiuliza kwanini sasa.
Baada ya kukusanya taarifa hizi kidogo nilipata maswali kadhaa ya kujiuliza kama ifuatavyo:-
1. Je STEPS ENT kitendo chake kinavunja sheria yoyote ?
2. Je STEPS ENT kitendo chake kinawezaje kuvunja ushindani na kupelekea kufariki makampuni mengine?
3. Je makampuni mengine yakiuza CD kiasi cha shilingi 1500/= (ikiuzwa maximu kwa wanunuzi) yanaweza kupata faida nakushindana sokoni?
4. Je wasanii/wanaolalamikia kwamba steps imewabana kwenye bei wanatakiwa kufisha malalamiko yao wapi?
5. Je kitendo cha Wizara kuuizuia kampuni ya STEPS ENT kisheria kiko sawa?
JE STEPS ENT. ILIVUNJA SHERIA YOYOTE
Kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani namba 08/2002 (fair compepetition act 2003). Kifungu cha 3 cha sheria ya hiyo lengo lake ni kwamba
1. Increase efficiency in the production distribution and supply of goods and service.
2. Promote innovation
3. maximize the efficient allocation, distribution of supply
4. Protect customers.
Lengo la sheria hii kama ilivyoanishawa kwa mujibu wa kifungu cha 3 kama lengo la kutunga sheria hii ni1. kuongeza uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma,2. kukuza ubunifu ,3.kuongeza ufanisi katika usambazaji 4.kuwalinda walaji au wanunuzi wa bidhaa au huduma.
Lengo kuu kabisa ni kuongeza wigo wa ajira na kuwalinda wanunuzi lakini ajira hizo lazima ziwe na taratibu za kisheria pale inapotokea mgongano wa kimaslahi.
Pia kwa mujibu wa sheria hiyo neno competition in markets (ushindani katika soko) litafsiriwa kama 'as dominant position in a market." (kuhodhi soko) Kifungu cha 5 competition means competition in a market refers to the process whereby:-
1. Supply or attempt to supply the same or substitutable goods or service to the persons in the same relevant geographical market, or
2. Acquire or attempt to receive the same or substitutable goods or service from the persons in the same relevant geographical market.
3. Markets mean a market in TZ or a part of TZ and refer to the range of reasonable possibilities for substitution in supply or demand between particular kinds of goods or service and between supplies and acquires or potential supplies or acquires of those goods or services.
Kwamba kwa mujibu wa kifungu hiki ni wazi kuwa unaposema ushandanikatika soko inaaminisha kwamba:-
1. Kujaribu au kusambaza bidhaa inayofanana au kutoa huduma inayofanana kwenye eneo moja la kijographia ya soko ,
2. Kushikika/ kupata au kujaribu kupokea bidhaa kutoka kwa mtu au watu wa eneo mmoja la jiographia ya biashara,
3. Soko inaamanisha ni soko aidha taznania au sehemu ya Tanzania sehemu ambayo katika umbali ambao kuna mahitaji ya bidhaa na hupatikana, bidhaa kwa maana ya huduma, usambazaji etc
Kwa mujibu wa kifungu cha 6 kinasema kwamba mtu anakuwa amehodhi soko ikiwa:-
a) Acting alone, the persons can profitably and materially restrain – reduce competition of that market for significant period of time and
(b) The person's share of the relevant markets exceeds 30%.
Kwa mujibu wa kifungu hiki endapo mtu atakuwa atakuwa yupo sokoni pekee yake na akazuia wengine kwa kipindi Fulani kwa kupunguza shindani au anamiliki zaidi asilimia 30% ya soko soko lote, huyo atakuwa maehodhi soko.
Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (1) 'kinakataza kutumia nguvu kuua ushindani sokoni;-
1. Kwa mujibu wa vifungu vyote hivi ni wazi kwamba STEPS ENT hajavunja sheria yoyote kwa sababu, alichofanya ni kupunguza bei kwenye filamu zake na wanacholalamika wasanii /wasambazaji ni kwamba upungzaji huo una lengo la kuuwa shindani na kasha STEPS ENT. baki peke yake sokoni, japo kimantiki STEPS ENT kama hajavunja sheri yoyote ile kwa kupunguza bei huko, lakini kwa mujibu wa WASAMBAZAJI WEnGINE hoja yao ya kwamba STEPS ENT itabaki mwenyewe sokoni itakuwa na mashiko pale watakapoweza kwenda kufungua shauri lao katika BARAZA LA USHINDANI ambapo watawasilisha hoja zao na baraza hilo kwa mujibu wa kifungu cha 11 (supra) kufikia maamuzi kitafanya uchunguzi wake ikiwemo kwenda sokoni/ kweye maduka na kuongea na pande zote na wadau wa hiyo sekta na kisha kutoa maamuzi yake.
2. WIZARA husika kuzuia kampuni ya STEPS ENT. Kuuza CD zao kwa bei walioipanga ni wazi kwamba kinakwenda kinyume na sera ya soko huria , hata hoja zao walizozitoa hazina mashiko wala mantiki (nukuu) kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu. Maoni yangu kwamba uhalisi wa bei hiyo unaweza tu kutolewa maamuzi na BARAZA LA USHINDANI ikikumbukwe hakuna bei elekezi katika filamu pili suala kwamba itasababisha tasnia kudharauliwa sio kweli hata kidogo kimtazamo wangu tasnia haiwezi kushuka au kudharauliwa kwa Cd kuuzwa bei hiyo, bali itadharauliwa kwa kutoa kazi zisizo na ubora.
Walichokifanya STEPS ENT kinafanywa pia na bank, mfano kwa sasa NBC inariba ya 18 % kwa mikopo yake yote itoayo kwa watumishi wa umma , wakati POSTA 23% na CRDB 19%, ndio soko huria linavyokwenda. Steps nao wanaweza kwenda ku challenge maamuzi ya wizara Mahakamani kama yanakwenda kinyume na sera ya soko huria mabyo ndio inaysimamiwa na nchi.
Kwa mujibu wa wa taarifa nilizozipata STEPS ENT. inasmekana ana mtambo ambao anaweza kutoa CD moja kwa moja na hivyo yeye kutoingia gharama za kununua CD tupu, ambayo inafika Tshs 240, kwa kila CD. Kwa mujibu wa chanzo hicho gharama za kutengneza CD ni kama ifuatavyo KAVA 60,KASHA 270,CD240 =570, kwa mantiki hiyo STEPS akiuza kwa bei yta jumlya 1000/= yeye anauwezo wa kutengeneza CD kwa jumla ya shilingi 330. Katika bei ya 1000 yeye anaweza kuapata Tshs 670/= wakati wasambazaji wemgine wanaweza kupata Tshs 430/= kwa kila CD.
Mwisho kabisa niseme kwamba akina MTITU wasiichukulie issue personal bali waichukulie kama kazi na biashara na wasihusishe na mambo mengi kuwataja akina JB, MZEE MAJUTO ,RITCHIE wakati wao ni waajiriwa wa kampuni nadhani sio sawa, huu ni mgogano wa kimaslahi kama JB na wenzake wameajiriwa kwa mikataba STEPS ENY halali hakuna hata ya kuwajumuisha kwenye hili wao kama waajiriwa. Suala la wasanii wenyewe kwa ridhaa yao kuuza CD kazi zao mimi nadhani suala hili kisheria sio kosa japo wanahaki ambazo wanatakiwa wapate hata wakiuza kazi zao.
PILI Mtitu ajaribu kukaa katika point 1 yeye ni msanii kwenye hili au ni Msambazaji na je maslahi ambayo anajaribu kuyapigania yanuhusiano wa moja kwa moja na wasanii au wasambajazji.
TATU STEPS ENT, watu wao kama BOND BI NN SINAN aache kutuia majibu rahisi kwenye maswai magumu kwani kufananisha sinema za ulaya jinsi zilivyochezwa na bei inayouzwa hapa TZ je ni kweli CD hizo zinazouzwa hapa ni halisi au zimeghushiwa na hao maharamia, jibu lipo wazi tatu STEPS ENT. wawe wakweli je kitendo chao kinaweza kitaondoa uharamia au kitabadiisha aina ya uharamia, au tuamini kwamba wanakusudia kuua ushindani sokoni.
Kwamba katika suala hili nilionavyo kwamza pande sizitafute mshindi bali zitafute haki, na pili maono yangu ni kwamba pande zote zina hoja zenye mashiko hivyo waende kwenye vyombo vya sheria.
Mwandishi wa makala hii OTHUMAN ROLENZA ni mfuatiliaji wa sekta hii ya burudani.
(ADVOCATE, PUBLIC SERVANT AND RESERCHER (law, political science and economic diplomacy).
DSM
Saluti5 haijapunguza wala kuongeza neno katika makala hii, imewekwa kama ilivyo. Kama wewe ni mdau na mfuatiliaji mgogoro huu na una mawazo yako tofauti na haya ya OTHUMAN ROLENZA, unakaribishwa kuleta makala yako Saluti5 kupitia email:sajmdoe@yahoo.com
Comments
Post a Comment