Liverpool imeenaza kuwa tishio kwa timu zinanyatia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kupata ushindi mwingine muhimu dhidi ya Aston Villa.
Ikicheza ugenini, Liverpool ikatandaza soka safi na kuvuna ushindi wa bao 2-0 huku kocha wa Aston Villa, Paul Lambert akizidi kupata shinikizo kwa mashabiki wa timu hiyo.
Wakati Aston Villa ikienda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao la dakika ya 24 lililofungwa na Fabio Borini, mashabiki wenyeji waliojazana kwenye uwanja wa Villa Park, walimzomea kocha huyo kuonyesha kukerwa kwao na ukame wa ushindi.
Hadi sasa Aston Villa hajapata ushindi katika jumla ya masaa 8 na dakika 42 katika mechi mbali mbali ilizoshiriki.
Rickie Lambert aliyetokea benchi ndiye aliyekuwa mwiba zaidi kwa Aston Villa baada ya kupachika goli la pili dakika ya 79.
Aston Villa: Guzan 7.5, Hutton 6,5, Okore 6, Baker 6, Cissokho 5, Sanchez 7, Westwood 5 (Gil 5, 59), Delph 6.5, Cleverley 4 (Weimann 6, 59), Agbonlahor 4, Benteke 6
Liverpool: Mignolet 7.5, Can 8, Skrtel 7.5, Sakho 6.5, Markovic 6.5, Moreno 6.5 (Enrique 6, 71), Lucas 7.5, Henderson 8, Sterling 6.5 (Ibe 85), Coutinho 8.5, Borini 7 (Lambert 7, 71)
Comments
Post a Comment