Na Bertha Lumala, Dar es            Salaam 
          Kiungo Mrundi Pierre Kwizera amejiunga na Sofapaka FC ya            Ligi Kuu ya Kenya (KPL), imefahamika.
Kwizera alitemwa Simba SC dakika za mwisho za usajili wa dirisha dogo msimu huu (Desemba 14, 2014) pamoja na Mrundi mwenzake Amisi Tambwe ili kuwapisha Waganda Simon Sserunkuma na Juuko Murshid.
George Banda, meneja wa mchezaji huyo, amesema Kwizera atatua Kenya kesho akitokea kwao Burundi ingawa kumeibuka utata katika upatikanaji wa Uhamisho wa Kimataifa.
Utata uliooibuka katika kupata ITC ya nyota huyo umeelezwa na Banda kuwa walipowasiliana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo mchana wameambiwa ilipetumwa klabu ya Rayon ya Rwanda.
"Mimi kama meneja wa Kwizera, ninajua hajasaini wala kuzungumza na Rayon FC. Ninashangaa kuambiwa na TFF kwamba ITC ya Kwizera iliyumwa Rwanda," amesema Banda.
Comments
Post a Comment