KWA LUCAS SILVA REAL MADRID IMELAMBA DUME


KWA LUCAS SILVA REAL MADRID IMELAMBA DUME

Klabu ya Real Madrid inatarajajiwa kutakata zaidi katika eneo la kati baada ya kukamilisha usajili wa kiungo Lucas Silva kutoka kutoka Cruizero ya Brazil kwa kitita cha pauni millioni 11.

Mchezaji huyo wa miaka 21 ambaye alifanyiwa ukaguzi wa afya siku ya jumatatu, ameweka sahihi ambayo itamuweka katika Real Madrid hadi Juni 30 mwaka 2020.

Kiungo huyo anatajwa kama mmoja wa viungo wa hali ya juu wanaoinukia barani Amerika ya Kusini. Ana uwezo wa kumiliki mpira pamoja na mbinu kali za ukabaji.

Silva knows how to please the Madrid faithful as he              kisses the jersey on his unveiling at the Bernabeu

Silva ameiwakilisha Brazil katika soka ya chini ya umri wa miaka 21 na kuisadia Cruizero kushinda mwaka 2013 na 2014.

 



Comments