Onyesho la Extra Bongo Jumanne usiku pale Flamingo Bar Magomeni Mwembechai lilihuhudhuriwa na wasanii wengi wakiwemo wanamuziki wa dansi.
Miongoni mwanamuziki wa dansi waliokuwepo ni rapa J4 na mwimbaji Kalala Jr kutoka Twanga Pepeta, Twaha Malovee wa Msondo, Amos na Ferguson wa Mashujaa Band bila kusahau mzee mzima Mafumu Bilal Bombenga wa African Beat.
Aidha, mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Bushoke naye alikuwepo huku mwigizaji Ben Branco naye akiwa ndani ya nyumba.
Hali kama hiyo inatokea katika maonyesho ya bendi nyingi ambako wasanii wa bendi tofauti huwa na kawaida ya kwenda kuwaunga mkono wenzao kadri nafasi inavyowaruhsu, jambo linaloonyesha kuwa wanamuziki wote ni ndugu moja licha ya upinzani wa kibiashara wa bendi zao.
Pichani ni Kalala Jr akifuatialia kwa makini onyesho hilo la Extra Bongo. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Hamis Boha na katikati ni mwigizaji Ben Branco.
Comments
Post a Comment