Timu zikiingia Uwanjani CCM Kirumba Jijini Mwanza, Tayari kwa mpambano wa Ligi kuu Vodacom Kati ya wenyeji Kagera Sugar vs Mbeya City.
Waamuzi wa Mtanange Timu Kepteni walipata picha ya Pamoja.
Kocha wa Mbeya City akipongezana na Kipa wake leo baada ya mpira kumalizika kwa Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Kagera Sugar Mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM-Kirumba Jijini Mwanza. Bao la pekee la Ushindi la Mbaya City lilifungwa dakika ya 84 na Peter Mapunda baada ya kuwatoka mabeki wa Kagera na kufunga bao hilo ambalo kiujumla lilisababishwa na kujisahau kwa mabeki wa Kagera Sugar.
Tawira ya Mashabiki kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Mbeya City wameifunga Kagera Sugar, wanaotumia Uwanja huo kwa Mechi za Nyumbani baada Kaitaba kufungwa kwa ukarabati, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 84 la Peter Mapunda.
Mashabiki wa Mbeya City waliokuja kutoka Jiji la Mbeya kuja Mwanza kuwapa sapoti wenzao
Benchi la Mbeya City
Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi akiangalia Vijana wake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mashabiki wa Mbeya City.
Wadau wa Soka wakiiendelea kuingia Jukwaa kuu katika uwanja wa CCM Kirumba
Mdau na mwandishi wa Blog ya Gsengo.blogspot.com wa jijini Mwanza akipata picha ya Pamoja na kiongozi wa Mpira Mjini hapa Mwanza.
Mashabiki wakiutazama mpira kwa hamu kubwa wa Ligi Kuu Vodacom Jijini Mwanza.
Mashabiki wa Mbeya City katika jukwaa kuu wakitazama matanange
Juma Mwambusi na Msaidizi wake wakiteta jambo
Nani kuugusa wa kwanza!!
Mchezaji wa Mbeya City akimbana wa Mchezaji wa Kagera Sugar
Mchezaji wa Mbeya City akiondosha mpira kenye eneo la hatari
Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia bao baada ya Timu yao kupata bao katika dakika za Mwishoni dakika ya 84.
Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi akihojiwa na Baadhi ya Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa Kaitaba jioni ya leo baada ya Timu yake kuibuka na Ushindi wa bao 1-0 Dhidi ya Kagera Suagar ya mjini Bukoba. Picha na Faustine Ruta wa Bukobasports.com
Raha ya Ushindi
Comments
Post a Comment