Kocha wa Fiorentina Vincenzo Montella ameuambia mkutano wa waanidishi wa habari nchini Italia kuwa wamemuuza rasmi mshambuliaji wao Juan Cuadrado kwa Chelsea ya England.
Kwa mujibu wa ripoti, Cuadrado bado yuko Italia lakini ataruka kwenda London kukamilisha vupimo vya afya Jumamosi kabla hajakamilisha usajili wake wa pauni milioni 23.3
Alipoulizwa juu ya usajili wa Cuadrado kwenda Chelsea, Montella alisema Ijumaa mchana: "Ni mauzo ambayo yameshakamilika.
"Cuadrado ni mchezaji aliyewasili hapa kwa tabasamu na akajitoa kwa kila kitu kwaajili ya Fiorentina.
"Ninashawishika kuwa kama Chelsea itataka kumtumia Jumamosi, basi anaweza akacheza. Nina furaha kwa vile anakwenda klabu kubwa."
Comments
Post a Comment